OSMkilawiki 419

2018-08-03

24.07.2018-30.07.2018

About us

  • OSMKilaWiki sasa inachapiswa katika Kikorea. Kikorea kinazungumzwa na watu wapatao milioni 80, hasa katika Korea lakini pia ni lugha rasmi katika mikoa miwili ya Kichina. Habari zinazohusiana na OSM sasa zinaweza kusomwa kwa Kijapani, Kicheki, Kiingereza, Kihispania, Kifaransa, Kijerumani na Kikorea. Kwa mujibu wa Tweet Pia kutoka kwa Geoffrey Kateregga kutakuwa na toleo la Kiswahili la suala hili hivi karibuni. Swahili inazungumzwa na watu milioni 50 hadi 100 nchini Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Msumbiji na Kongo. 고급 협동 조합 na Geoffrey bado wanatafuta washirika watakaowasaidia. OSMkilawiki inatafuta bendera bora ya kutumia kwa lugha ya Kikorea katika plugin ya WordPress qTranslate.

SotM 2018 Milan

  • [1] State of the Map, Mkutano wa kimataifa wa OpenStreetMap(SOTM), ulifanyika Milan, Italy wikendi iliyopita kuanzia tarehe 28 hadi 30, mwezi wa Julai 2018. Unaweza tazama video zilizorekodiwa katika kituo chao cha YouTube channel na picha zote hapa.

  • Tunataka kuwapongeza washindi wa Tuzo za OSM 2018:

  • Katika mkutano wa kimataifa wa SotM Martijn van Exel alizindua toleo jipya la tovuti la ImproveOSM.

  • Kutoka SotM Milan 2018: maelezo ya jumla ya shughuli za siku ya kwanza kutoka mawasilisho mbalimbali.

  • Kwa niaba ya kampuni ya Mapbox, Jinal alisema walivyosubiri sana kuona watu Milan katika mkutano wa kimataifa wa SOTM. Lakini ikiwa hukupata wakati, au unaishi mbali na Italy, Jinal anapendekeza baadhi ya mikutano mingine ya OSM ambapo waweza kukutana na wawakilishi wa kampuni ya Mapbox.

  • Katika OSM blog, Harry Wood anasema shukrani kwa wageni na waandaaji wa SotM huko Milan. Tayari kuna video zilizorekodiwa ambazo hazijatangiwa kwenye vyumba viwili vya mkutano mkuu ambavyo vilihusishwa kwenye makala.

  • Wakati wa SotM mkataba wa makubaliano kati ya OSGeo Foundation na YouthMappers ilisainiwa. Mkataba huo unapendekeza kuanzisha uhusiano wa ushirikiano katika maeneo kadhaa kama utafiti, elimu na ushiriki wa mkutano.

OSGeo ni shirika ambalo linaendeleza kupitishwa kwa teknolojia ya geospatial huria, YouthMappers ni muungano wa vyuo vikuu 120 katika nchi 38 zinazofanya kazi katika sekta ya kibinadamu na maendeleo.

  • Mkutano wa kimataifa wa SotM mwaka ujao, 2019 utafanyika mjini Heidelberg, Germany!

Mapping

  • Ni nadra sana kwa majadiliano ya OSM kubadilika haraka kama ilivyofanyika katika orodha ya barua pepe ya talk-us kuhusu mistari kutoshikamana ambazo zilitakiwa kuwa barabara.

  • Jgon6 hakuamini kwamba hakuna njia shawishi ya kutambulisha viwanja vya kuonyesha. Alikumbuswa na aliangalia suala hilo tena. Aliandika barua pepe kwa “tagging mailing list” na akachapisha diary ambayo aliweka mawazo ya kina na matokeo kuhusu njia tofauti zakufanya hivo ili watu wengine watoe maoni/ mitazamo yao.

Community

  • Toleo la nane la Open Summer of Code wa Ubelgiji ulimalizika wiki iliyopita. Ilikuwa kubwa zaidi kuliko hapo awali na ilitumia OpenStreetMap sana, kama ilivyoonyeshwa na post ya Diary Vander Vennet.

  • Tunasubiri kuona matukio ya utafiti ya profgreenington. Anaelezea zaidi katika chapisho lake la diary

  • Richard Fairhurst aliandika blog post kuhusu kutekeleza vector tiles, na kuweka hatua hii ya kati kwa maelezo kamili ya mazingira ya OSM. Alikumbuka siku za kwanza za OSM, kwa muhtasari wa hali ya sasa, alibainisha hoja ya mara kwa mara ya kuwa OSM ni database na si ramani, na akasisitiza kwa nini OSM si na wala hatutaki kuwa kama ramani za Google au Apple. Pia aliongea juu ya msukumo wa kuwa na mchanganyiko wa wachangiaji tofauti ili kujadili vector tiles za kurejesha kwenye openstreetmap.org kama chombo cha kuzalisha ramani zilizoboreshwa. Makala pia inatoa maneno yenye utulivu kuhusu kujifunza AI katika mazingira ya OSM na maoni kwenye ramani kama msukumo wa wafadhili.

OpenStreetMap Foundation

  • Raphael Das Gupta akaribisha tawi za OSM kujiunga na orodha ya barua pepe. Ushirikiano na kubadilishana uzoefu kati ya tawi za OSM ni muhimu, pamoja na ushirikiano na Bodi ya OSMF na makundi mbalimbali ya kazi.

Events

  • Wito wa eneo la kufanyia State of the Map Africa 2019 sasa limefunguliwa. Tarehe ya mwisho ya kutuma ombi hili ni Septemba 30, 2018.

  • FOSS4G na HOT Summit itafanyika Dar es Salaam, Tanzania kutoka Agosti 27 hadi Septemba 2, 2018. Mkutano huu utaleta pamoja watumiaji, teknolojia na watengenezaji wa teknolojia.

Humanitarian OSM

  • Mazungumzo ya HOT katika SotM 2018: unaweza kupata orodha kamili ya mazungumzo, kuhusu OSM na shughuli za kibinadamu hapa. Ikiwa umepoteza mmoja wao au unataka kuifanya upya tena, video na slides zitapatikana kwenye ukurasa huu huo.

  • [HOT] Tukio la Ebola imeripotiwa tena katika DRC, angalia kazi 4947

switch2OSM

  • Ripoti ya habari ya Moneycontrol kwamba Uber inafanya kazi kwenye mpango wa kuhamisha kutoka kwenye ramani za Google hadi OSM. OSMkilawiki hivi karibuni imeripoti mpango wa Uber kuchangia OSM katika eneo la Delhi nchini India.

Programming

  • Wiki ya OSM sasa inatumia templates zilizoandikwa katika lugha ya Lua scripting. Inatarajia kuwa hii itaimarisha utendaji na kudumisha wa templates ambazo hutumiwa mara kwa mara, kama vile bar ya uteuzi wa lugha.

Releases

  • Waazilishi wa JOSM wamechapisha toleo #14066, itakayokuletea marekebisho na uborefu.

Did you know …

  • Pahali pa usaidizi ukiwa na swali kuhusu OSM? Waweza uliza swali lako katika jukwaa la OSM, katika orodha ya barua pepe) na pia kwenye tovuti ya Q & A help.openstreetmap.org. Tovuti hii haijabuniwa kwa minajili ya majadiliano kama ilivyo jukwaa na orodha ya barua bali kwa maswali ya hakika ambayo yana lengo la kupata jibu sahihi. Ikiwa una tamanio la kusaidia wengine na maarifa yako ya OSM, tazama orodha ya maswali ambayo hayajajibiwa. Pengine unafaa kuwa pahali kwenye orodha ya points.

Other “geo” things

  • Shirika la habari Bloomberg rinaripoti kwamba Mapbox inadai kuwa na jukumu katika siku zijazo za magari ya kukimbia na ya kujitegemea. Pamoja na wateja wake Uber na mpinzani wake Lyft, Mapbox tayari imeweka na mguu kwenye mlango wa teknolojia ambayo inaonekana kama baadaye ya uhamaji.

Upcoming Events

undefinedundefinedundefinedundefined
StuttgartStuttgarter Stammtisch2018-08-01Germany
BochumMappertreffen2018-08-02Germany
BalatonőszödBalatonőszöd-Balatonszemes mapping party2018-08-04-2018-08-05Hungary at Lake Balaton
Buenos AiresMapatón-taller OSM2018-08-04Argentina
Amagasakiみんなのサマーセミナー:地図、描いてますか?描きましょう!2018-08-05Japan
LondonMissing Maps Mapathon2018-08-07United Kingdom
MünchenMünchner Stammtisch2018-08-08Germany
UrspringStammtisch Ulmer Alb2018-08-09Germany
Berlin122. Berlin-Brandenburg Stammtisch2018-08-10Germany
Tokyo東京!街歩き!マッピングパーティ:第22回 富岡八幡宮2018-08-12Japan

Hii OSMKilaWiki imetolewa na Kateregga1, Laura Mugeha, Nakaner, Polyglot, rogehm, Spanholz, derFred, doktorpixel14, odetteaida.


Leave a reply

Comments loading…